Njia Mpya Ya Asili Ambayo Imewasaidia Maelfu Ya Wanawake Kama Wewe Kupungua Uzito Na Kuondoa Kitambi Na Manyamazembe Bila Ya Mlo Mkali Wala Mazoezi Magumu
Mpendwa msomaji
Kama unataka kupungua Uzito na Kuondoa Kitambi na Manyamazembe Kirahisi Kupitia Njia Salama na ya Uhakika bila ya mazoezi magumu au kula vyakula vya aina fulani tu
Hata kama ulijifungua kwa upasuaji au hata kama umekuwa ukijaribu njia mbalimbali bila ya mafanikio …
Ili uanze kuwa na mwili imara, wenye nguvu na wa kuvutia….
Na kuondokana na karaha za kupewa majina ya kejeli na kujichukia mwenyewe na hatimaye uanze kujipenda na kuwa rafiki wa kioo ….
Huku ukiachana na ulazima wa kuvaa nguo pana kwa lengo la kuficha kitambi na manyamazembe na badala yake uanze kuvaa nguo zako pendwa zilizokuwa zimekubana …
Na kufurahia kutembelea maduka ya mavazi ili kujipatia nguo za mishono ya kisasa (fashion) bila kikwazo cha maumbile
Huku ukifurahia kuvaa kila aina ya nguo uipendayo na hata viatu vyenye kisigino kirefu hali itakayobadili hadi mwondoko wako na kuufanya uwe wa kisasa zaidi …
Si hivyo tu bali pia mwonekano wako uweze kurudi nyuma hadi kwa miaka 15 na kuwa kama binti mrembo mwenye sura ya ujana zaidi, ngozi nyororo, laini na ng’avu ….
Kiasi cha kumvutia kila atakayekutazama na hasa mwenzi wako bila ya kupoteza pesa zako kwa kununua vipodozi na cream zenye gharama kubwa
Na hivyo kuokoa pesa nyingi zitakazokusaidia kufanya manunuzi ya lazima na kuepuka kuharibu ngozi yako kwa vipodozi na cream zenye kemikali…
Jambo ambalo litakufanya ujiamini, ujipende na kujisikia vizuri kushiriki mambo ya kijamii ikiwemo sherehe, mitoko, vikao ....
Bila kuwa na wasiwasi wa kutengwa au kuzungumziwa vibaya na hivyo kurejesha fursa zilizokupita kutokana na mwonekano usiovutia ….
Na kikubwa zaidi Afya yako iwe bora zaidi kwa kuepuka magonjwa yanayotokana na uzito mkubwa
Hasa magonjwa ya shinikizo la juu la damu, kisukari, maradhi ya moyo, maumivu ya viungo, mvurugiko wa homoni na kukosa usingizi au kukoroma uwapo usingizini ….
Hivyo uyafurahie maisha na kuepuka gharama kubwa za matibabu ambazo hayana suluhisho la kutibu isipokuwa kutuliza
Na hivyo kutumia bajeti ambayo ingeenda kwenye matibabu kwa kufanya majukumu mengine ya kifamilia.
Basi unatakiwa kusoma kila neno kwenye ukurasa huu kwa sababu
Unaelekea Kugundua Njia Mpya Na Ya Kipekee Ambayo Itapelekea Changamoto Yako Ibaki Kuwa Historia.
Njia Hii Ni Asilia, Rahisi, Ya Kudumu, Haichoshi Na Salama Kwa Afya Yako Kwani Haina Madhara Yoyote Mwilini Na Imefanyiwa Tafiti Za Kina, Majaribio Ya Kisayansi Na Kuthibitishwa Na Mamlaka Za Afya Za Kimataifa Kuwa Ni Njia Bora Zaidi Na Salama Yenye Uwezo Mkubwa Wa Kuleta Matokeo Na Kukufanya Uanze Kuona Mabadiliko Ndani Ya Siku 7
Naitwa Mwalimu Rehema Paul. Ninawasaidia wanawake kuondokana na changamoto ya uzito mkubwa, kitambi na manyamazembe kwa kuwapatia Elimu sahihi .......
Elimu ambayo inahusu 'Jinsi ya kuondokana na changamoto hiyo na kuzuia isijirudie tena kupitia njia salama asilia bila ya mazoezi magumu, lishe kali (strict diet) wala kumeza vidonge
Ni ukweli ulio wazi kuwa kila mwanamke anajivunia kuwa na mwonekano wa ujana zaidi na mwili wenye umbo linalovutia kwa kila anayemtazama.
Nikiwa kama mwanamke mwenzako ninajua ni kwa jinsi gani changamoto ya uzito mkubwa, kitambi na manyamazembe inakuwazisha na hata kukukosesha usingizi…
Kwa sababu mtu wangu wa karibu alikuwa akipambana na Uzito, kitambi na manyamazembe kwa muda mrefu kama wewe.
Nina uhakika kama ilivyokuwa kwa mtu wangu huyu wa karibu hata wewe pia umejaribu njia mbalimbali za kuweza kuondokana na uzito mkubwa, kitambi na manyamazembe .......
Lakini licha ya jitahada zote ambazo umekuwa ukifanya umeishia kupoteza pesa na muda wako kwenye njia ambazo hazikupi matokeo unayotamani kuyapata.
Tazama, kama wanawake wengine, mtu wangu huyu wa karibu amewahi kutumia njia mbalimbali ikiwemo virutubisho lishe, dawa za asili na vidonge mbalimbali vya kupunguza uzito ....
Cha kustaajabisha ni kwamba kila alipomaliza kutumia kila mojawapo ya njia hizo uzito wake ulikuwa ukirudi tena na mara nyingine ulirudi hata zaidi ya mwanzo jambo ambalo lilikuwa likimchanganya zaidi
Si hivyo tu bali pia alijiunga na madarasa ya jinsi ya kupunguza uzito ambako alifundishwa kutumia lishe kali 'strict diet' na kufanya mazoezi magumu yaliyomlazimu kwenda gym kwa matumaini kwamba hatimaye angeweza kufanikiwa
Hata hivyo huko nako mambo yalimuwia magumu zaidi kwani njia hizo zilikuwa na ugumu wa kuzingatia na hazikuendana na mwili wake na hali yake ya kiafya.
Cha kusikitisha zaidi ni kwamba kila alipomaliza mafunzo ya lishe kali na mazoezi magumu uzito nao ulianza kurejea tena. Ni kana kwamba, kila hatua ya mbele ilirudi nyuma mara mbili asijue ni wapi alipokuwa akikosea…
Zaidi sana madarasa aliyojiunga yalikuwa na walimu ambao hawakulenga kuelewa changamoto zake binafsi kama vile upasuaji aliofanyiwa, tatizo la kisukari, shinikizo la juu la damu na ratiba ngumu ya kila siku.
Na pia hawakuweza kumfuatilia kwa karibu jambo lililosababisha ajihisi kuwa yuko peke yake katika safari yake ya kupungua uzito na hivyo mabadiliko yalikuwa yanaonekana taratibu sana hali ambayo ilimvunja moyo kabisa.
Nikamshauri mtu wangu huyu wa karibu asikilize ushauri wangu na kuufanyia kazi kwani ni wa uhakika na salama kuweza kumsaidia kuondokana na changamoto yake na kuzuia isirudi tena lakini hakutaka kuamini maneno yangu
Badala yake akaendelea kujaribu ushauri mwingine mara nyingi zaidi ambapo licha ya kuwekeza pesa nyingi kwenye ushauri aliopatiwa kila mara alihisi kutopata thamani ya pesa zake kwani hakuna kilichokuwa kinafanya kazi kwa muda mrefu.
Hadi kufikia hapo alihisi amemaliza njia zote na zote zikiwa zimegonga mwamba na kumuacha akijisikia vibaya na kuhisi uzito wa mwili wake ukiathiri kila kitu—kutoka kujiamini hadi afya yake
Kwa aibu, akiwa mpole sana akanifuata na kuniambia sasa niko tayari kusikiliza ushauri wangu na kujaribu njia yangu.
Alipokubali kusikiliza ushauri wangu na kujiunga na darasa langu hakika mtazamo wake ulibadilika.
Sikumlazimisha kufanya mazoezi magumu, badala yake nilimfundisha mbinu rahisi na asilia ambazo aliweza kuzitekeleza bila kubadilisha maisha yake ghafla.
Nilimsaidia kugundua sababu za kisaikolojia na kiakili zilizokuwa zikimkwamisha.
Kwa mara ya kwanza, mtu wangu huyo wa karibu alipata msaada binafsi wa karibu huku nikimfuatilia hatua kwa hatua kuhakikisha kuwa anaendelea kuwa na motisha na kujiona akifanikiwa.
Matokeo yalikuja kwa kasi na kwa mara ya kwanza alihisi kuwa safari yake ya kupunguza uzito haikuwa ngumu sana na ingeweza kudumu.
Baada ya wiki moja tu, alianza kuona mabadiliko yaliyompa hamasa ya kuendelea kwani alianza kujihisi kuwa na mwili mwepesi na kuanza kuvuta pumzi vizuri.
Na baada ya wiki 3, mabadiliko yakaongezeka huku nguo zilizokuwa zikimbana sana zikianza kuingia mwilini, ngozi ikaanza kung’aa na kuwa nyororo na maumivu ya miguu kupungua kwa kiasi kikubwa huku akizidi kuwa mchangamfu na mwenye nguvu zaidi
Hadi kufikia wiki ya 4, mabadiliko yalimshangaza sana asiamini macho yake, tayari alikuwa amepunguza kilo 7 tumbo limenywea na manyamazembe kupungua kwa kiasi kikubwa…
Nguo zilizokuwa zimejaa kabatini kwa sababu ya kumbana akaanza kuzivaa bila ya mazoezi magumu, bila kumeza vidonge vya kupunguza uzito wala kutumia virutubisho lishe vya makampuni na bila kutumia strict diet (lishe kali)
Huku hali ya sukari na shinikizo la juu la damu ikikaa vizuri licha ya kuzembea maelekezo kwa baadhi ya siku
Akiwa na furaha isiyoelezeka, wiki ya 6 aliamua kwenda kupima uzito na kujikuta ameondoa kilo 10 jambo ambalo lilikuwa ni muujiza mkubwa kwake
Na hapo sasa kila aliyemjua alikuwa akimshangaa jinsi ambavyo amekuwa na mwonekana wa kuvutia na Wafanyakazi wenzake ofisini wakimsumbua kwa kutaka kujua siri ya mabadiliko yake.
Hadi sasa ni miaka 3 uzito haujarudi, kitambi hakijatokeza wala manyama zembe au dalili yoyote ile ya kurudi alikotoka.
Leo hii, mtu wangu huyo wa karibu si tu kwamba amepungua uzito na kuondoa kitambi na manyamazembe bali mwili wake umekuwa imara, wenye nguvu, mchangamfu na afya
Huku mwonekano wake ukiwa wa ujana zaidi, ngozi nyororo, laini na inayong’aa kiasi kwamba hata mume wake anamtamani
Anafurahia kuvaa nguo za mishono mbalimbali, suruari za jeans, kuchomekea blauzi na kuvaa viatu virefu. Kiufupi anajipenda, anajiamini, mwenzi wake anamfurahia, afya yake imekuwa nzuri na ameokoa bajeti kubwa ya matibabu
Si hivyo tu, bali pia ameweza kubadili mtindo wa maisha yake.
kiufupi ni kwamba anaendelea kufurahia matokeo aliyoyapata bila hofu ya kurudi kwenye uzito wa awali.
Pengine unatamani kujua ndugu yangu huyu alitumia njia gani ambayo imemsaidia kuondokana na karaha ya kitambi, manyamazembe na uzito mkubwa, usijali!
Ndani ya dakika 2 zijazo nitakuambia alitumia njia gani lakini kwanza unatakiwa ujue kwamba
Tafiti Za Kisayansi Zinaonesha Kwamba Hadi Mwaka 2023 Zaidi Ya Watu Bilioni Moja Duniani Kote Walikuwa Na Changamoto Ya Uzito Mkubwa Na Unene Kupita Kiasi ‘Obesity’ Idadi Kubwa Zaidi wakiwa Ni Wanawake
Kati yao milioni 880 ni watu wazima na idadi imekuwa ikiongezeka kwa kasi kila mwaka kwani kutokea 1975 hadi 2023 idadi imeongezeka mara tatu.
Kwa data hizi inakadiriwa kuwa hadi 2035 huenda nusu ya watu wazima wote duniani wakakumbwa na changamoto hii na idadi kubwa zaidi ikiwa ni ya wanawake kutokana na maumbile yao.
Jambo la kustua ni kwamba uzito mkubwa na ‘unene’ ndicho chanzo cha matatizo makubwa ya Kiafya hasa maradhi hatari yanayoshika nafasi ya kwanza kwa kuchangia vifo vingi duniani ukiachana na ajali…
Maradhi hayo hatari ni pamoja na shinikizo la juu la damu (high blood pressure), kisukari type 2, moyo kutanuka, moyo kushindwa kufanya kazi vizuri (heart failure), mshtuko wa moyo (heart attack), kiharusi (stroke) na baadhi ya kansa
Pia ugumu wa kupata uja uzito, maumivu ya viungo, kupoteza kumbukumbu, kukosa hamu ya kujamiiana, kukosa usingizi, kukoroma usingizini, unene kupita kiasi (obesity), matatizo ya ini na figo, kupumua kwa shida,
Na hata mvurugiko wa homoni (hormonal imbalance) , msongo wa Mawazo 'stress' na sonona 'depression'
Na kati ya wote wenye changamoto ya uzito mkubwa na unene nusu yao (50%) madhara hayajaanza kuwaletea shida kwa kiasi kikubwa na wakati nusu iliyobaki ni ambao madhara yameshaanza kuleta shida kubwa
Kwa hiyo kama hujaanza kupata madhara yoyote makubwa yanayotokana na uzito mkubwa na unene tambua kwamba upo kwenye kundi la watu ambao madhara hayajaanza kuwaletea shida kubwa
Lini madhara hayo yataleta shida kubwa? Hakuna anayejua, ni Muda wowote - Unaweza ukaanza kupata shida. Miili inatofautiana kwa wengine madhara yanajitokeza kwa kiwango kikubwa sana na kwa haraka wakati wengine madhara yanajitokeza kwa kiwango cha wastani na kwa taratibu.
Taarifa mbaya ni kwamba...
Japokuwa tafiti zimefanyika kujua kisababishi cha uzito mkubwa, kitambi na manyamazembe
Lakini kwa kuwa tatizo hili limekumba watu wengi sana duniani kote na kusababisha uhitaji mkubwa wa watu kutafuta suluhisho la haraka….
Basi imechukuliwa ni kama fursa kwa makampuni, viwanda na hata wafanya biashara binafsi kuwekeza na kufanya biashara ya kujitajirisha kupitia bidhaa za aina mbalimbali
Kwa madai kwamba ni bidhaa zinazosaidia kutatua changamoto ya uzito, kitambi na manyamazembe pasipo kuwekeza muda wa kufanya tafiti na majaribio ya bidhaa hizo ili kupata njia ya uhakika ....
Na hivyo kusababisha uwepo wa mfumuko wa watu wenye uzito mkubwa, kitambi manyamazembe na matumizi ya bidhaa zenye kemikali hatari
Cha kusikitisha ni kwamba njia nyingi sio salama kwani zina madhara mabaya kwa mtumiaji kama vile kushusha kinga ya mwili, kudhoofu afya, nyama za mwili kulegea, mwonekano wa uzee na msongo wa Mawazo.
Mbali na njia hizo zisizo salama, njia nyingi sio endelevu kwani Licha ya kusaidia uzito kupungua na kitambi na manyamazembe kuondoka lakini matokeo yanadumu kwa muda mfupi tu na hii ni kwa sababu zina ugumu wa kuzingatia
Ndio sababu kwa miaka mingi sasa watu wamekuwa wakihangaika kutumia njia mbalimbali bila ya mafanikio na wengine kufikia hatua ya kukata tamaa kabisa huku idadi ya watu walioathirika ikiongezeka kwa kasi kubwa
Sasa kama nilivyokuambia japokuwa tafiti zimefanyika kujua kisababishi cha uzito mkubwa lakini imekuwa vigumu kupata njia zenye uhakika wa kutatua changamoto hiyo
Sababu kubwa ikiwa tatizo hili limechukuliwa ni kama fursa ya kibiashara kwa watu kujitajirisha tu badala ya kuwekeza kwanza kwenye tafiti za kupata njia ya uhakika itakayomaliza tatizo.
Ili njia ya uhakika ipatikane ni lazima pawepo na tafiti za kina zinazofanyiwa majaribio ya kutosha na kisha kuthibitishwa kisayansi kuleta matokeo sahihi bila ya kusababisha madhara kwa mtumiaji
Chanzo Cha Kugunduliwa Kwa Njia Iliyomsaidia Mtu Wangu Wa Karibu Mpaka Akapungua Uzito, Kitambi Na Manyamazembe Na Kuzuia Hali Hiyo Isijirudie Tena
Mwezi wa 3 mwaka 2015 nilianza rasmi kazi ya kuuza virutubisho Lishe kama wakala wa Kampuni moja kubwa kutoka Afrika kusini.
Japokuwa kulikuwa na aina nyingi za virutubisho lishe lakini niliamua kujikita kwenye Virutubisho Lishe vya kupunguza uzito, kitambi na manyamazembe kwani niliona ni changamoto inayowanyima usingizi na amani wanawake wengi zaidi
Lakini, haikuchukua muda mrefu kugundua kuwa wanawake wengi niliowauzia virutubisho lishe hivyo walikatisha dose kutokana na gharama kubwa ya angalau shilingi 1,400,000 kwa miezi 3 mfululizo
Si hivyo tu, baadhi yao walichoshwa na idadi ya vidonge walivyotakiwa kumeza kila siku kutwa mara tatu. Na wengine kuhofia kuwa huenda vingewaletea madhara licha ya kuwaelimisha kuwa ni salama.
Baada ya miezi 7 hivi wale waliokuwa wamefanikiwa kukamilisha dose ya miezi 3 na kufurahia matokeo walinipigia simu wakilalamikia kuona uzito ukianza kurudi tena na tumbo kuanza kuchomoza baada ya miezi 4 tu.
Na huku wakinilalamikia nyama za mwili kulegea na hivyo kupoteza mvuto.
Huduma niliyoianza kwa matumaini makubwa ilibadilika kuwa mwiba, kwani badala ya kupokea simu za shuhuda nzuri za kupungua, nikawa mtu wa kusikiliza malalamiko kila kukicha.
Jambo hili lilinikosesha amani kabisa hata kukosa usingizi, nikijiuliza kama nilikuwa naumiza wateja wangu kwa kuwashauri kununua bidhaa ambazo hatimaye hazikuwapa matokeo ya kudumu.
Uamuzi Wa Kubadili Njia Na Kutafuta Suluhisho La Kudumu
Mwaka 2017 nilichukua uamuzi mgumu wa kuacha kushauri watu watumie virutubisho Lishe ili kupungua uzito na kuondoa kitambi na manyamazembe na badala yake niliwashauri watumie dawa za asili.
Njia hii ilinipa matumaini kwa kuwa vitu vya asili ni bora zaidi lakini pia gharama ya dawa hizo ilikuwa ndogo ukilinganisha na ile ya Virutubisho Lishe kutoka nje ya nchi
Kwani njia hii ya vidonge vya asili ilikuwa shilingi 30,000 Tu kwa dose ambapo mteja alitakiwa kumeza kidonge kimoja kila siku na kupungua haraka hadi kilo 20 ndani ya mwezi mmoja.
Sikuchukua hatua ya haraka kwani ilinibidi nifuatilie kwanza kupata ukweli na shuhuda kwa waliozitumia, shuhuda zilionesha kupungua ndani ya muda mfupi sana kiasi kwamba ilinishangaza, nikaona kwa kuwa watu wanataka kupungua kwa haraka hapa sasa nimefika.
Hata hivyo, baada ya kuwashauri wanawake hao watumie dawa hizo za asili furaha yangu haikudumu kwani dawa zilikuwa zimetengenezwa kwa mimea ambayo ilikuwa ikisaidia kutoa mafuta kupitia kuharisha sana
Na pia ilikuwa ikisababisha hali mbalimbali ikiwemo kichefuchefu kikali, kutapika, asidi, tumbo kujisikia kujaa na kukata.
Japokuwa hali hizi zilidumu kwa muda mfupi baada ya kumeza kidonge lakini ilisababisha ugumu wa kukamilisha dose kwa sababu ilimuwia vigumu mtumiaji kutoka na kuendelea na majukumu yake kutokana na kuharisha sana
Lakini pia nyama za mwili zililegea na kwa waliojitahidi kumaliza dozi (japo kwa shida) haikuchukua muda mrefu uzito ulianza kurudi tena na suala la malalamiko likawa pale pale.
Hakika nilijisikia mnyonge na kuhisi kukata tamaa ya kuendelea na lengo langu la kusaidia wanawake kuondokana na changamoto ya uzito, kitambi na manyamazembe.
Kupata Suluhisho La Uhakika, Bora, Salama Na Asilia:
Nikiwa katika hali ya kukata tamaa, siku moja wakati nimepumzika kitandani huku nikiperuzi peruzi mtandaoni nikakutana na Makala yenye kichwa cha habari kilichosema...
‘Jifunze Jinsi Ya Kupungua Kilo 10 ndani Ya Siku 40 Kupitia Njia Salama, Asilia, Ya Kudumu Na Uhakika Bila Ya Mazoezi Magumu wala kumeza vidonge’
Nilishtuka na sikuamini macho yangu. Lakini nikaamua kuisoma kwa sababu makala hiyo ilikuwa bure kabisa.
Mwandishi wa makala hiyo alikuwa Bwana mmoja kutoka nchini Marekani akielezea jinsi ambavyo aligundua njia iliyomsaidia kupungua uzito na unene na kupona shinikizo la juu la damu baada ya kuteseka kwa miaka mingi.
Kwa jinsi ambavyo njia hiyo ilionekana kuwa rahisi, nilihisi kama naota. Nilijiuliza: “Hivi kweli jambo dogo kama hili linaweza kuwa suluhisho?”
Kilichoniaminisha na kunivutia ni wingi wa shuhuda za wanawake waliokuwa wakifurahia kupungua haraka kwa kufanya mabadiliko madogo tu na wengine wakisema ni miaka 4 sasa uzito haujarudi wala kitambi au manyamazembe.
Sasa nirudi kwenye Makala ya huyo Bwana, aliandika hivi…
Akiwa anakaribia kukata tamaa ya kuendelea kuishi kutokana na unene na kuugua kwa miaka mingi ndipo alipogundua jambo ambalo liliwastua watu wengi kiasi cha kuwa na hofu ya kile ambacho kingetokea kufuatia ugunduzi huo.
Kwani aligundua kuwa karibia kila kitu alichokuwa ameshauriwa na madaktari wa Afya na wataalamu wa Lishe na Mazoezi hakikuwa sahihi kabisa hivyo kusababisha tatizo lake la uzito na shinikizo la juu la damu kuongezeka.
Akiwa katika hali ya kuchanganyikiwa aliamua kuchukua hatua ya kuacha kuwasikiliza wataalam hao wa lishe na mazoezi na hata madaktari wake wote waliokuwa wakimtibu
Na badala yake aliamua kuzama kwa kina katika kufanya Tafiti na kujifanyia majaribio kwenye mwili wake kama vile panya wanavyofanyiwa tafiti kwenye maabara za kujifunza tabia na magonjwa ya binadamu
Haikuwa rahisi kwani ilimchukua muda mrefu sana hadi pale alipougundua ukweli.
Kilichomsaidia Bwana huyo kuujua ukweli ni pale alipofanya kinyume kabisa na ushauri aliokuwa amepewa halafu Afya yake ikaboreka sana.....
Kwani shinikizo la juu la damu likashuka na akapona matatizo mengi yaliyotokana na hali ya uzito mkubwa na bila ya kutumia nguvu Bwana huyu alifanikiwa kupungua kilo 10 ndani ya siku 40.
Baada ya matokeo hayo alisema hivi, ninanukuu “Watu wengi ambao wanatoa ushauri kuhusu Lishe na mazoezi ni watu ambao hawajapitia changamoto ya uzito mkubwa wala kuwa wanene (kitambi na manyamazembe)
Kamwe hawatakuonesha picha zao zinazoonyesha kabla ya kupungua uzito na baada ya kupungua uzito kwa sababu hawajawahi kuwa hivyo
Lakini mimi nina picha za kabla na baada ya kupungua uzito kwa sababu nimekuwa huko”
Alikiri kuwa kilo 10 alizopungua ndani ya siku 40 hakufanya mazoezi kabisa.
Na jambo lililomshangaza zaidi ni kwamba haikuwa jambo gumu au la kuumiza bali ilikuwa ni kitu cha kufurahisha na kizuri.
Washauri wake wa lishe na mazoezi na madaktari waliokuwa wakimtibu walibaki midomo wazi kufuatia ugunduzi wake!
Na haya ni baadhi tu ya mambo ambayo yalitokana na ugunduzi huo:
Kwanza kabisa alitunukiwa Tuzo ya mshindi namba 1 katika kuelimisha watu Jinsi ya kupungua uzito na kuchoma mafuta kupitia njia salama na za kuaminika
Si hivyo tu bali pia alitunukiwa nishani ya muuzaji bora wa Makala za Afya kwenye majarida ya New York Times
Na nishani ya mshindi namba 1 kwenye vipindi maalum vya Television vinavyomhoji kuhusu Tafiti zake.
Huu ni mwaka wa 11 Bwana huyo akiendelea kudumisha matokeo aliyoyapata
Hivi ninavyoongea Njia yake aliyoigundua ndiyo inayoshika nafasi ya kwanza kwenye mataifa makubwa 8 dunia huko barani Ulaya na Marekani
Na ndio njia ya kipekee ambayo ni salama na ya uhakika kwa kuleta matokeo makubwa, mazuri na ya kufurahisha ndani ya muda mfupi kadiri iwezekanavyo
Kwani tangia wakati huo hadi leo hii shuhuda zimekuwa zikimiminika kwa wingi watu wakifurahia mabadiliko ya kushangaza baada ya miaka mingi ya mahangaiko ambayo hayakuzaa matunda
Na hata wanawake ambao uzito ulikuwa umegoma kupungua kwa sababu ya kukosekana kwa usawa wa homoni licha ya jitihada mbalimbali walizofanya kwa muda mrefu wakitumia muda na pesa nyingi hadi kujikatia tamaa
Hao nao pia walishangazwa jinsi walivyobadilika kwa haraka
Na sasa ndio njia inayotumiwa na watu maarufu wakubwa duniani ambao wanavutia wakiwemo ma - star wa muziki, uigizaji na watangazaji wa television (celebrates)
Mwishoni mwa Makala yake Bwana huyo alitangaza kozi ya kulipia ili kujifunza zaidi jinsi ugunduzi huo unavyofanya kazi
Japokuwa gharama ya kujiunga na kozi hiyo ilikuwa pesa nyingi sababu malipo yalikuwa kwa dola, lakini sikusita kulipia na kuwekeza muda wa kujifunza japo haikuwa kazi rahisi kama ambavyo nimekurahisishia wewe.
Haya hapa Matokeo Niliyoyapata Baada Ya Kujifunza Mbinu Hii Kutoka Kwa Huyu Bwana Wa Marekani.
Kutumia Mbinu Mpya kwa Wateja Wangu Matokeo ya Ajabu!
Baada ya kujifunza nilianza kujaribu njia hii mpya na ya kipekee kwa wateja wangu wa Virutubisho Lishe
Ambapo nilianza kwa kuwapatia Elimu ya kula vyakula rahisi, vitamu na asilia na kupunguza au kuacha baadhi ya tabia na vyakula vilivyokuwa vikiwazuia kupungua uzito...
Na huku wakibadili mtindo wa maisha kidogo kidogo.
Wakati huo huo nikiwa nawaza huenda mambo yakawa yale yale ya kupokea malalamiko toka kwa watumiaji lakini cha kushangaza safari hii mambo yalikuwa kinyume kabisa na hapo awali.
Kwani Matokeo yalikuwa ya kufurahisha mno! Baadhi ya Wateja walishuhudia kupungua hadi kilo 10 ndani ya siku 30 bila dawa, bila virutubisho Lishe na bila ya mazoezi magumu.
Hakika ilikuwa shangwe na ushindi mkubwa kwangu, kwani ndoto yangu ya kupata suluhisho la kweli la kusaidia watu kupungua uzito na kitambi na manyamazembe ilikuwa imebadilika na kuwa kitu halisi
Sasa wateja hao wakaanza kuniletea marafiki zao, simu zikawa nyingi za kutaka huduma yangu.
Hapo ndipo nilipowaza kuwa ili kurahisisha kazi ya kuwahudumia na ili niweze kufikia watu wengi zaidi wenye changamoto ya uzito nitumie mitandao ya kijamii ‘Instagram, whatsApp na Facebook’
Kwa hiyo nilichukua hatua nyingine ya kununua kozi ya jinsi ya kutangaza na kutoa elimu kupitia mitandao ya kijamii.
Nikiri kuwa haikuwa kazi rahisi lakini pamoja na ugumu uliokuwepo ikiwemo kuwekeza muda na pesa niliweza kufanikisha.
Mwezi Februari, mwaka 2021 Nilianza rasmi kuendesha madarasa kupitia mtandaoni, nikifundisha kuhusu njia rahisi na za kuaminika za kupunguza uzito na kuondoa kitambi kwa kula vyakula vya asili na kubadili mtindo wa maisha
Ambapo kwa gharama ndogo tu watu wengi walijiunga na madarasa yangu
Matokeo ya Madarasa Yangu: Afya Bora, Mwili Imara Wa Kuvutia Na Furaha Zaidi
Sasa, watu wanapungua kilo 7 hadi 10 ndani ya siku 30 hadi siku 40
Hii ikimaanisha kuwa wengine wanawahi zaidi kupata matokeo na wengine wanapata baada ya muda mrefu zaidi kulingana na mwitikio wa mwili, nidhamu ya kufuata maelekezo na shauku ya kupata matokeo
Cha kufurahisha zaidi ni kuwa mwonekana unabadilika kabisa na kuwa wa ujana zaidi , nyama zilizokaza, uchangamfu na nguvu zaidi huku wakila chakula ambacho ni kitamu na rahisi kupatika kwenye masoko yetu ya mitaani
Huku wakiendelea kufurahia Maisha pasipo uchovu, lishe kali, mazoezi magumu, kumeza vidonge wala malalamiko tena.
Si hivyo tu bali pia wanapata elimu ya jinsi ya kuzuia uzito kurudi tena na jinsi ya kuishi maisha yenye afya bora kupitia usaidizi wa karibu.
Hakuna kulalamika tena kuhusu kitambi kugoma kuondoka, kwa sababu elimu ninayowapatia inawawezesha kubadili kabisa mwili na afya zao kwa njia salama na ya kudumu.
Hadi sasa, nimeweza kusaidia zaidi ya wanawake 2,500 kuondokana kabisa na madhara yatokanayo na changamoto ya uzito mkubwa, kitambi na manyamazembe.
Kupitia mafanikio haya, nimepata utulivu wa akili, amani, na furaha ya kuona wateja wangu wakifurahia maisha yao wakiwa na afya bora zaidi.
Hapo ndipo nilipojua nimepata njia ya uhakika inayotatua changamoto ya uzito, kitambi na manyamazembe.
Njia aliyoigundua Bwana Huyo Kutoka Marekani Na Kupelekea Kupungua Kwa Haraka Na Kupona Kabisa Na Sasa Ni Miaka 11 Imepita Changamoto hiyo haijarudi Tena Ni
‘Program Ya Chakula Cha Mwitu’
Kama nilivyokuambia, Japokuwa tafiti zimefanyika kujua kisababishi cha uzito mkubwa lakini imekuwa vigumu kupata njia zenye uhakika wa kutatua changamoto hiyo na kuzuia isijirudie tena kwa sababu ya kukosekana kwa tafiti makini
Kilichomsaidia Bwana huyo kutoka Marekani kugundua njia yenye uhakika ni maamuzi yake ya kujikita kwenye tafiti hadi alipofanikiwa kugundua ukweli wa njia ya uhakika isiyo na madhara yoyote kwa mtumiaji
Ugunduzi ambao ulipelekea agundue kanuni za kisayansi ambazo zinazingatia njia asilia. Nitakueleza njia hiyo inavyofanya kazi hapo mbeleni,
Kwa sasa ngoja tuongelee kitu kilichosababisha wewe uongezeke uzito na kuwa na kitambi na manyamazembe. Hii ni muhimu kwa sababu ukijua chanzo utaelewa ugunduzi huo utakavyokusaidia kutatua changamoto yako
Uzito mkubwa, Kitambi na manyamazembe ni jambo linalosababishwa na Mlundikano wa Mafuta yaliyohifadhiwa mwilini (Japokuwa vitu kama taka mwili pia vinachangia uzito lakini ni kwa kiasi kidogo na ni rahisi tu kuziondoa)

Kila Kitu Kinachozalishwa Mwilini Lazima Kina Chanzo Chake. Kwa hiyo Ngoja Nikuoneshe Chanzo Cha Mlundikano wa Mafuta Yaliyohifadhiwa Katika Mwili Wako Ni Kipi!
Kwa kuwa kinachosababisha uzito, kitambi na manyamazembe ni Mlundikano wa mafuta yaliyohifadhiwa mwilini
Hivyo basi ili kuzuia uzito mkubwa, kitambi na manyamazembe kwenye mwili wako unatakiwa kujua kinachosababisha mlundikano huo wa mafuta yaliyohifadhiwa mwilini ili uweze kukidhibiti.
Ukiweza kukidhibiti chanzo cha mlundikano wa mafuta yaliyohifadhiwa kwenye mwili wako utakuwa umefanikiwa kuzuia ongezeko la uzito, kitambi na manyamazembe.
Na baada ya kudhibiti mafuta yasiendelee kuhifadhiwa mwilini kinachobaki ni kuyeyusha mafuta ambayo tayari yalishahifadhiwa mwilini.
Kwa kufanya hivyo, kitambi manyamazembe na uzito vinakwisha na unakuwa na uhakika wa kutopata tena uzito mkubwa, kitambi na manyamazembe tena kwa sababu unakuwa umedhibiti mafuta yasiendelee kuhifadhiwa
Swali la kujiuliza ni kwamba...
Mafuta yanahifadhiwa vipi mwilini na nini chanzo chake mwilini?
Mlundikano Wa Mafuta Mwilini Ni Kama Mafuta Ya Alizeti Ambayo Ni Matokeo Ya Kukamuliwa Kwa Mbegu Za Alizeti Mashineni
Ili upate mafuta lazima mashine izisage na kuzikamua hizo mbegu za alizeti ili zigeuzwe kuwa mafuta. Kama mashine ikisaga na kukamua mbegu nyingi za alizeti yatapatikana mafuta mengi. Na mashine ikisimama kukamua mbegu za alizeti au ikipunguza kasi ya kukamua mbegu za alizeti maana yake mafuta hayatapatikana au yatapatikana kidogo.
Kwa mfano huo ndivyo ilivyo kwenye ongezeko la mafuta mwilini. Ili mafuta yawepo mwilini lazima mashine ya mwili (homoni) iitwayo Insulin igeuze glucose (mbegu za alizeti) kuwa mafuta
Baada ya glucose (mbegu za alizeti) kugeuzwa kuwa mafuta, mafuta hayo ndio yanahifadhiwa sehemu mbalimbali mwilini na hasa tumboni...
Na kadiri Insulin (mashine) inavyoendelea kugeuza kiasi kikubwa cha glucose (mbegu za alizeti) kuwa mafuta ndivyo ambavyo mafuta yanapatikana kwa wingi na kuhifadhiwa kwa kiasi kikubwa zaidi
Na hivyo kusababisha mlundikano mkubwa wa mafuta yaliyohifadhiwa mwilini hadi kupelekea tumbo kuchomoza (kitambi) na manyamazembe kwenye sehemu zingine mwilini hatimaye uzito kuongezeka pia.
Sasa basi, wa kuwa mlundikano wa mafuta yaliyohifadhiwa mwilini ndio kisababishi kikuu cha uzito mkubwa, kitambi na manyamazembe, na kinachogeuzwa kuwa mafuta ni glucose (mbegu za alizeti)
Njia rahisi ya kudhibiti ongezeko la mafuta mwilini ni kudhibiti kiasi cha glucose (mbegu za alizeti) ili insulin (mashine) isimamishe au ipunguze kasi ya kugeuza glucose kuwa mafuta.
Ni wazi kuwa mashine (insulin) ikisimamisha au ikipunguza kasi ya kugeuza glucose (mbegu za alizeti) kuwa mafuta, hakutakuwa na mafuta yanayohifadhiwa na kama yatakuwepo basi ni kwa kiasi kidogo mno ambacho hakitakuwa na madhara mabaya mwilini.
Kama Una Uzito Mkubwa, Kitambi Na Manyamazembe ‘Glucose’ Sio Rafiki Yako Mzuri
Tazama, kisababishi Kikuu cha uzito mkubwa, kitambi na manyamazembe ni mlundikano wa mafuta yaliyohifadhiwa mwilini (na glucose ndio kitu pekee kinachobadilishwa kuwa mafuta)
Kwa hiyo unaweza ukaona kwamba Glucose sio rafiki yako mzuri…
Kwa sababu asipodhibitiwa ataendelea kubadilishwa kuwa mafuta ambayo yatapelekea kuwa na uzito, kitambi na manyamazembe mpaka hatua ya kusababisha maradhi hatari kwa afya na umbo lisilovutia
Bwana huyo kwa kuligundua hilo alifanikiwa kugundua ‘Program Ya Chakula Mwitu’
Jambo la kwanza ambalo Program hii inakwenda kulifanya ni kudhibiti kiwango cha Glucose kwenye damu ili kwamba Insulin isimamishe kazi ya kubadili glucose kuwa mafuta
Insulin ikishasimamisha kubadilisha glucose kuwa mafuta kazi inayobakia ni ya kuyeyusha mafuta ambayo tayari yalishahifadhiwa ili kitambi na manyamazembe viondoke na hatimaye uzito nao upungue.
Kabla sijaeleza jinsi 'Program Ya Chakula Mwitu' inavyofanya kazi hebu tuangalie mambo manne yanayosababisha kiasi cha glucose kuwa kikubwa zaidi kwenye mwili wako
Kitu kinachosababisha Kiasi Cha ‘Glucose’ Kuwa Kikubwa Zaidi Kwenye Damu Yako
Kwanza kabisa unatakiwa kujua kuwa Glucose ni ya muhimu mwilini kwa sababu ni chanzo kimojawapo cha nguvu/nishati mwilini.
Viungo vyako vyote kama vile ubongo, moyo, mapafu, misuli, macho vinahitaji nguvu ili viweze kufanya kazi kwa kiwango kinachotakiwa kama vile kupumua, kutembea, kuona na kufikiri
Sasa tujiulize kama glucose ni ya muhimu, kwa nini isiwe rafiki yako?....
Glucose inavunja urafiki na wewe pale ambapo itazalishwa kila baada ya muda mfupi na kwa kiasi kikubwa zaidi kuliko kiasi knachohitajika kwenye mwili wako
Sasa tuangalie mambo hayo 4 yanayosababisha uwepo wa kiasi kikubwa zaidi cha Glucose kwenye damu hadi kupelekea kuhifadhiwa kama mafuta….
Jambo la kwanza ambalo linachangia kwa kiasi kikubwa zaidi cha takribani 80% ni Lishe: Nitaeleza:
Unapokuwa na tabia ya kula vyakula na vinywaji vyenye kiasi kikubwa cha carbohydrates kwa maana ya wanga na sukari (na sio vyakula vyenye mafuta kwa wingi kama wengi wao wanaovyodhani)
Vyakula na vinywaji hivyo vyenye kiasi kikubwa cha carbohydrates vinapoingia mwilini vinameng’enywa kwa haraka na kubadilishwa kuwa glucose
Kisha glucose hiyo inafyonzwa kwa haraka na kuingia kwenye damu. Kwa hiyo Glucose ni sukari iliyoko kwenye damu.
Sasa tuangalie mchakato mzima unavyokuwa hadi mafuta yanahifadhiwa mwilini na kusababisha kitambi, manyamazembe na uzito.
Unatakiwa kujua kuwa uzito, kitambi na manyamazembe havitokei kufumba na kufumbua bali ni mchakato ambao uko katika hatua sita na mchakato huo unachukua muda mrefu wa miezi hadi miaka.
Ambapo hatua ya kwanza ni wewe kula vyakula (na vinywaji) vyenye kiasi kikubwa cha carbohydrates na baada ya kula chakula hicho......
Hatua inayofuata ambayo ni ya pili, chakula hicho ulichokula kinameng'enywa na kubadishwa kuwa glucose ambapo glucose hii inafyonzwa na kuingia kwenye damu yako na Ikishaingia kwenye damu inafuata hatua nyingine
Katika hatua hii ambayo ni ya tatu, Glucose iliyoko kwenye damu inatumika kama Nishati ya kuupatia mwili wako nguvu kuanzia seli hadi viungo vyako vyote vya mwili ikiwemo ubongo, moyo, misuli, mapafu ili viweze kufanya kazi
Mwili wako ukishatumia kiasi cha glucose kinachohitaji kwa wakati huo kiasi kingine kinasalia kwenye damu bila kazi yoyote.
Sasa basi kwa usalama wako ili kuzuia glucose iliyosalia kwenye damu isilete madhara kama ya kisukari type 2, ndipo inapofuata hatua ya nne ambapo Tezi yako ya kongosho inalazimika kuzalisha kiasi kikubwa zaidi cha Insulin na kukiingiza kwenye damu.
Insulin iliyoingia kwenye damu inafanya kazi ya kuondoa hiyo glucose iliyosalia kwenye damu ili isilete hayo madhara ya kisukari type 2.
Jambo la kustua ni kwamba.......
Ulaji wa Vyakula vyenye carbohydrates kwa wingi (sukari na wanga) vina tabia mbili, tabia ya kwanza ni kuupatia mwili nguvu ya haraka (shibe ya haraka) na njaa ya haraka (havishibishi kwa muda mrefu)
Kwa hiyo kila baada ya muda mfupi utasikia njaa na utakachokula tena ni aina hiyo hiyo ya chakula kwa sababu inatuliza njaa kwa haraka.
Na tabia ya pili ni kuathiri ubongo kwa kutengeneza ughaibu au uteja yani unakuwa ‘addicted’ kwa hiyo kila wakati unatamani kula kitu chenye sukari na wanga na hivyo kujikuta kila baada ya masaa 2 hadi 3 ukila chakula hicho
Tabia hizi mbili zinasababisha glucose kuzalishwa kila baada ya muda mfupi na kusababisha kupanda kwa glucose halafu Insulin inazalishwa kwa kiasi kikubwa kila inapopanda glucose ili kuondoa na kushusha kiasi cha glucose kilichozidi na kusalia kwenye damu
Kwa hiyo kitendo cha kupanda na kushuka kwa glucose kila baada ya muda mfupi kinatengeneza kitu kama umbo la mikunjo linaloitwa ‘Glycemic Roller coaster’
Glycemic Roller coaster (kupanda na kushuka kwa glucose) inasababisha uingie kwenye hatua ya tano inayoitwa mtego wa insulin ‘Insulin Trap’.

Ukishaingia kwenye mtego huo wa Insulin basi Insulin inafanya kazi kubwa mbili hapa ...
Kazi ya kwanza ni kuibadilisha glucose iliyoondolewa na kuibadilisha iwe mafuta.
Mafuta hayo yanasafirishwa kwa msaada wa insulin hadi kwenda kuhifadhiwa maeneo mengine mwilini hasa tumboni (fat storage increases) kama akiba ya baadaye endapo yatahitajika kutumika kama nishati
Na kazi ya pili ni kuzuia hayo mafuta yaliyohifadhiwa yasitumike kama nishati ya kuupatia mwili nguvu ambapo kitaalam tunasema mwili unaacha kuchoma mafuta (Fat Burning Stops) kwa sababu hakuna uhitaji wa Nishati ya ziada.
Jambo la msingi kukumbuka ni kwamba, mafuta yaliyohifadhiwa ni nishati ya ziada ambayo inaweza kutumika kuupatia mwili nguvu kunapokuwa na upungufu wa glucose kwenye damu.
Maeneo Ambayo Mafuta Yanahifadhiwa Mwilini
Kuna Maeneo 2 mwilini ambapo mafuta yanahifadhiwa
Eneo la kwanza ni lile lililopo ndani zaidi linalozunguka viungo (Organs) muhimu ambavyo viko ndani zaidi mwilini ikiwemo moyo, ini, figo, bandama, mapafu, mishipa ya damu na utumbo.
Mafuta yanayohifadhiwa eneo hilo la ndani zaidi kuzunguka viungo muhimu yanaitwa ‘Visceral Fat’ .
Kwa kawaida huwa hayaonekani kwa macho isipokuwa kwa vipimo vya kitaalamu na ndiyo mafuta hatari kwa Afya yako kwa kusababisha maradhi sugu kama vile magonjwa ya moyo, shinikizo la juu la damu, kisukari na baadhi ya kansa.
Eneo la pili ni kwenye tabaka la chini la ngozi. Aina hii ya mafuta inaitwa subcutaneous fat na unaweza kuyaona kwa macho unapofinya tumbo au unapojiangalia na kuona tumbo kubwa na manyama-nyama
Aina hii ya mafuta haina hatari kubwa kwa afya yako isipokuwa yanaathiri mwonekano wako kwa kusababisha kitambi na manyamazembe sehemu za kuzunguka kiuno, mapaja, hips, makalio na mashavu na kuchangia ongezeko la uzito.

Habari mbaya ni kwamba kwenye tabaka la ngozi hakuna kitu kama vile mifupa na viungo kinachoweza kuyazuia yasiendelee kuongezeka kama ilivyo kwenye visceral fat.
Hali hii ya kutokuwepo na kizuizi inapelekea hatua ya 6 ambapo mafuta yataendelea kuhifadhiwa na kulundikana zaidi na zaidi kadiri unavyoendelea kula carbohydrates
Na hapo sasa ndio tumbo linachomoza (kitambi) na wakati mwingine hadi kuning’inia na mengine yatahifadhiwa sehemu za kuzunguka kiuno, mapaja, hips, makalio na mashavu (manyamazembe).
Sasa hebu tuangalie jambo la pili linalosababisha uwepo wa kiasi kikubwa zaidi cha Glukose kwenye kwenye damu
jambo lenyewe ni kukosekana kwa usawa wa homoni (hormonal imbalance) kwenye mwili wako. Nitaeleza;
Homoni (Vichochezi) ni kemikali zinazozalishwa mwilini na kusafiri kupitia damu hadi kwenye ogani au viungo mbalimbali ili kutuma taarifa za kuchochea kazi mbalimbali zifanyike mwilini.
Homoni zote kwa pamoja zinafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa kuhakikisha michakato ya mwili inaenda vizuri
Kemikali hizi zinapozalishwa aidha kwa kiasi kidogo zaidi au kikubwa zaidi kutegemeana na aina ya homoni ndipo zinasababisha kukosekana kwa usawa wa homoni mwilini ‘hormonal Imbalance’
Japokuwa mwili wako una homoni zaidi ya hamsini, lakini zinazohusika zaidi kusababisha Glucose ipande ziko nane ambazo ni Insulin, Thyroid, Cortisol, Leptin, Leghin, Dopamine, Adiponectin na estrogen.
Sasa hebu tuangalie kazi ya kila homoni na chanzo cha kukosekana kwa usawa wa kila homoni (aidha kuwepo kwa kiasi kikubwa zaidi au kidogo zaidi) na jinsi kiasi hicho kinavyosababisha uwepo wa kiasi kikubwa cha glucose kwenye damu.
Tukianzia na homoni ‘Thyroid’ ambayo kazi yake kubwa ni kutawala mchakato mzima wa chakula mwilini (metabolism) baada ya wewe kula ikiwemo kuwezesha mfumo wa chakula kuwa na uwezo wa kubadili chakula ulichokula kiwe nishati (glucose) na kuwezesha nishati hiyo itumike kuupatia mwili nguvu
Thyroid inapozalishwa kwa kiasi kidogo kuliko kile kinachohitaji inasababisha seli za mwili kuwa na uwezo mdogo wa kutumia glucose iliyozalishwa kwenye damu kwa ajili ya kuvipatia viungo vya mwili nguvu hali inayojulikana kama ‘Insulin resistance’ .
Kwa hiyo seli zinaposhindwa kutumia glucose iliyopo kwenye damu ni wazi kuwa kutakuwa na kiasi kikubwa cha glucose kwenye damu
Kisababishi kikuu cha thyroid kuzalishwa kwa kiasi kidogo ni upungufu wa madini hasa madini ya iodine na hali nyinginezo za matibabu ya afya.
Ukiachilia homoni Thyroid, kuna homoni ‘Cortisol’ ambayo yenyewe huleta madhara inapozalishwa kwa kiwango kikubwa.
Kazi kubwa ya Cortisol ni kuzuia mwili usipate madhara makubwa yatokanayo na msongamano wa mawazo . Chanzo cha cortisol kuzalishwa kwa wingi ni msongamano wa Mawazo ‘stress’ hivyo inajulikana pia kama homoni ya stress
Cortisol inapozalishwa kwa kiasi kikubwa zaidi inasababisha mwili kutamani kula vyakula vya sukari na wanga (carbohydrates) ili kuupatia ubongo nguvu ya kufikiri. Unapokula carbohydrates kwa wingi basi kiasi kikubwa cha glucose kinazalishwa kwenye damu.
Kumbuka hapo awali nilisema vyakula vyenye kiasi kikubwa cha carbohydrates ndivyo ambavyo humeng'enywa na kugeuzwa kuwa glucose.
Homoni ‘Leptin’ ambayo pia inajulikana kama homoni ya shibe yenyewe inaleta madhara inapozalishwa kwa kiasi kikubwa halafu ikazuiliwa kufikisha taarifa za kushiba kwenye ubongo baada ya kula chakula.
Taarifa inaposhindwa kufika basi ubongo unazalisha homoni ya Ghelin (homoni ya njaa).
Sasa Ghelin ikizalishwa kwa wingi inakusababishia hali ya kujisikia kushiba kuondoka hata kama umekula chakula cha kutosha na hivyo kupelekea kula kupita kiasi vyakula vyenye carbohydrates ili kupooza njaa kwa haraka.
Matokeo ni carbohydrates kumeng’enywa kuwa glucose kila unapokula baada ya muda mfupi na kusababisha kiwango cha glucose kwenye damu kupanda sana.
Chanzo cha Leptin ni mafuta kuziba kwenye mishipa ya fahamu inayopeleka taarifa kwenye ubongo na chanzo cha ghelin kuzalishwa kwa wingi ni ubongo kushindwa kuwasiliana na Leptin.
Mbali na homoni hizo kuna homoni ‘Adponectin’ ambayo ikizalishwa kwa kiwango kikubwa inasababisha ‘Insulin resistance’ au insulin kupata ukinzani
Hali hii inasababisha seli za mwili kushindwa kufyonza kiasi cha kutosha cha glucose iliyozalishwa kwenye damu ili kuisambaza kwenye viungo mbalimbali mwilini na hivyo kusababisha kiasi cha glucose kilichopo kiendelee kuwepo kwenye damu na kuongezeka
Chanzo kikuu cha kuzalishwa Adponectin nyingi ni kemikali zinazoingia mwilini kupitia vyakula vilivyochakatwa, vinywaji, hewa chafu, mazingira, vipodozi na dawa zenye kemikali.
'Estrogen' ambayo ni homoni ya kike yenye kazi kubwa ya kuweka sawa maumbile ya kike na kuzuia mlundikano wa mafuta mwilinini inakuwa chanzo cha mfumuko wa unene kwa wanawake pale inapozalishwa kwa kiasi kidogo zaidi.
Visababishi vikuu vya estrogen kuzalishwa kwa kiasi kidogo ni umri, vipindi anavyopitia mwanamke ikiwemo kipindi cha kunyonyesha, kuelekea kukoma hedhi na kukoma hedhi (menopause) na lishe duni.
Mara nyingi tatizo linaanza kwenye umri wa miaka 25 mtu anapokuwa kwenye vipindi vya kunyonyesha ambapo tezi zinazalisha kiasi kidogo cha estrogen ili kuruhusu upatikanaji wa maziwa ya mama kwa kunyonyesha. Wakati huu mafuta hujikusanya zaidi kwenye hips na mapaja.
Na linakuwa kubwa zaidi kuanzia miaka ya 30 na hali kuwa mbaya kuanzia 40 na kuendelea wakati ambapo umri unasonga na kusababisha misuli ya mwili ilegee...
Misuli inapolegea haitumii nishati kubwa ya glucose nyingi, pia metaboliki au michakato ya mwili inapungua uwezo wa kufanya kazi na hivyo kusababisha uwepo wa kiasi kikubwa cha ziada ya glucose kwenye damu
Na inapofikia kuelekea vipindi vya kuelekea kukoma hedhi hadi kukoma hedhi tezi zinapunguza kuzalisha homoni estrogen kwa sababu hakuna utengenezwaji wa mayai.
Hivyo basi kiasi kidogo cha estrogen kinasababisha mwili ushindwe kuchoma mafuta na kusababisha mkusanyiko wa mafuta hasa maeneo ya tumboni.
Pia Lishe duni isiyo na mlo kamili hupelekea kuzalishwa kwa kiwango kidogo cha estrogen na kusababisha glucose kupanda . Ni kwa namna hii mwanamke anaongezeka uzito na anakuwa na kitambi na manyamazembe
Na homoni ya mwisho ni dapomine ambayo kazi yake ni kufanya ujisikie vizuri wakati unapokuwa na hisia (emotions) kama vile huzuni, upweke, hasira, stress.
Homoni hii inaamka pale unapokula vyakula na vinywaji vyenye sukari nyingi na chumvi nyingi. Kadiri unavyojisikia raha ukila ndivyo ambavyo unakula zaidi ili ujisikie raha zaidi.
Matokeo ya kula sukari kwa wingi ni kusababisah kiwango kikubwa cha glucose kuzalishwa kwenye damu au chumvi nyingi ambayo itasababisha kiasi kikubwa cha maji taka mwilini yanayoongeza uzito
Hadi hapo tumemaliza jambo la pili.
Sasa tuangalie jambo la tatu linalopelekea uwepo wa kiasi kikubwa zaidi cha Glucose kwenye damu
Jambo lenyewe ni Tabia ya kuketi kwa muda mrefu
Kumbuka nilisema jambo la kwanza ni Lishe na la pili ni kukosekana kwa usawa wa homoni. Na Sasa tuangalie jambo hili la tabia ya kutumia muda wako mwingi ukiwa umeketi.
Tabia hii inakukumba unapofanya kazi za mezani kama vile za kuandika au kutumia kompyuta au kuwa na watu wanaokufanyia sehemu kubwa ya kazi zako iwe kwenye biashara au nyumbani
Na wakati wewe huna tabia ya kutenga siku aidha za kufanya mazoezi mepesi japo mara 3 hadi 4 kwa wiki au kufanya kazi za nyumbani kama kunyweshea, kudeki na kusafisha mazingia
Unapotumia muda mwingi kuketi unaathiri utendaji kazi wa ubongo na Ubongo ndio kiungo kikuu kinachofanya kazi ya kutawala mifumo yote mwilini ikiwemo kuzalishwa kwa homoni za kutosha.
Ili ubongo ufanye kazi vizuri unahitaji oxygen ya kutosha, (oxygen ndio chakula cha ubongo na mifumo ya fahamu.) Ili oxgen iweze kuzunguka vizuri na kufika kwenye ubongo, ni lazima damu iwe inazunguka vizuri mwilini (damu ndio inazungusha oxgen)
Na ili damu iweze kuzunguka vizuri ni lazima moyo uwe na uwezo wa kusukuma damu na ili moyo uweze kusukuma damu ni lazima mwili uwe mchangamfu ‘active’ kupitia tabia ya kuvishughulisha viungo vyako aidha kwa kufanya shughuli kama za kutembea, kulima, kudeki, kusafisha mazingira
Au kwa kufanya mazoezi ya kawaida tu yanayosaidia kuchangamsha mwili
Zaidi ya hilo, Mwili usipokuwa mchangamfu (active) unasababisha kiasi kikubwa cha glucose kubaki kwenye damu kwa sababu hakuna nishati kubwa inayohitajika kuvipatia viungo nguvu.
Si hivyo tu bali pia usipokuwa active’ kwa kufanya kazi mbalimbali za kukuchangamsha au mazoezi misuli ya mwili inasinyaa. Inaposinyaa haitengenezi uhitaji wa nguvu nyingi kutoka kwenye glucose kwa hiyo kiasi kikubwa cha glucose kinabaki kwenye damu.
Na jambo la nne ni Kulala masaa machache
Ukilala chini ya masaa 6 unasababisha tatizo la kukosekana kwa usawa wa homoni (hormone imbalance) zinazohusika na ukuaji (growth hormone) ambazo zinafanya kazi ya kuchoma mafuta na kuzuia mlundikano wa mafuta mwilini.
Ntakupa mfano mmoja wa madhara ya kulala masaa machache; unasababisa kupanda kwa homoni ya stress ‘cortisol’
Cortisol ikipanda inasababisha hamu ya kula vyakula vyenye carbohydrates kwa wingi ili kuongezea ubongo nguvu ya kufikiri kwa muda mrefu kwa sababu huupatii nafasi ya kupumzika kutokana na kulala masaa machache.
Ukila carbohydrates kwa wingi unazalisha glucose kwa wingi.
Ili kuepuka hili unatakiwa kulala usiku walau muda usiopungua masaa 6 hadi 8 kila siku. Hii ni kwa sababu homoni au kemikali zinazalishwa wakati wa usiku unapokuwa umelala kwa muda wa kutosha.
Kwa hiyo ili uondokane na changamoto yako kabisa unatakiwa upate njia ambayo itafanya kazi ya kudhibiti kiasi cha glucose kwenye damu kisipande na kuzidi kiasi kinachotakiwa
Ukifanikiwa kuipata njia hiyo basi kupungua uzito, kuondoa kitambi na manyamazembe itakuwa rahisi kama kuyeyusha mafuta ya siagi kwenye kikaango cha moto.
Kwani tamaa ya kula vyakula vyenye sukari na wanga itakoma, njaa za kila baada ya muda mfupi zitakwisha, misuli ya mwili itajengeka, homoni zitakaa sawa, mwili wako utakuwa mchangamfu, na kupata usingizi wa kutosha
Ukweli Aliougundua Bwana Huyo Kwenye Tafiti Zake Na Majaribio
Sasa turudi kwenye tafiti zilizomwezesha Bwana huyo nchini Marekani kugundua ukweli.
Kama nilivyokueleza kuwa Bwana huyo alipewa ushauri ambao haukumsaidia na badala yake ulizidisha matatizo. Ushauri ambao ulimtaka ale vyakula vyenye kiasi kidogo cha mafuta ‘Low fat’, vyakula vyenye kiasi kidogo cha cholesterol
Si hivyo tu bali pia afanye mazoezi ya kukimbia kila siku umbali mrefu kwa muda wa saa moja.
Na baada ya kufanya utafiti wa kina aligundua kuwa njia hizo alizoshauriwa ziliwa chanzo cha yeye kuongezeka uzito, kunenepa zaidi na kuendelea kuugua shinikizi la juu la damu (High Blood Pressure)
Kumbuka Bwana huyu alishauriwa kula chakula chenye kiasi kidogo cha mafuta kama vile maziwa yenye kiasi kidogo cha mafuta 'low-fat milk', jibini yenye kiasi kidogo cha mafuta 'low fat cheese', na siagi yenye kiasi kidogo cha mafuta 'low fat butter.'
Katika tafiti zake aligundua kuwa vyakula hivyo vyenye kiasi kidogo cha mafuta ni vyakula ambavyo vina kiasi kikubwa cha carbohydrates (wanga na sukari).
Kwa hiyo yeye kula vyakula hivyo alikuwa akisababisha kiwango kikubwa cha glucose ambacho kilibadilishwa kuwa mafuta na kumsababishia ongezeko na unene, uzito na kuugua.
Yani Alichokifanya ilikuwa kinyume kabisa na ukweli
Si hivyo tu pia vyakula vyenye kiasi kidogo cha cholesterol kama vile mayai, nyama na nazi’. ambapo katika tafiti zake aligundua kuwa kuna aina mbili za cholesterol
kuna ambayo ni mbaya kwa sababu inaganda kwenye mishipa ya damu na kuna ambayo ni nzuri kwa sababu haigandi kwenye mishipa ya damu na badala yake inasafisha mishipa ya damu
Kwa hiyo vyakula alivyokatazwa vilikuwa na cholesterol nzuri ya kumsaidia tatizo lake la shinikizo la damu
Na pia vyakula hivyo ndivyo vinazuia ongezeko la glucose kwenye damu na kuzuia asiingie kwenye mtego wa Insulin ‘Insulin Trap’ kwa hiyo alichokuwa ameshauriwa ni kinyume kabisa.
Na umbali mrefu wa kukimbia kwa saa moja kila siku katika tafiti zake aligundua kuwa kufanya mazoezi kama adhabu kulisababisha homoni ya stress inayoitwa cortisol kupanda zaidi.
Ilipopanda ilimsababishia tamaa ya kula vyakula vyenye sukari na wanga kila baada ya muda mfupi na kuangukia kwenye kiasi kikubwa cha glucose na mtego wa Insulin ‘Insulin Trap’.
Kwa hiyo basi katika tafiti zake alizama kuujua ukweli na kilichomsaidia kujua ukweli ni pale alipofanya kinyume kabisa cha ushauri aliopewa na wanaojiita wataalamu na lishe na madaktari wa moyo
Jambo ambalo lilimpatia mabadiliko mazuri kwa haraka yaliyomsaidia kupungua kilo 10 ndani ya siku 40 kupitia Lishe tu bila ya mazoezi na kupona shinikizo la juu la damu.
Jinsi Ambavyo ‘Program Ya Chakula Mwitu’ Inafanya kazi.
Sasa tuangalie Jinsi ambavyo njia aliyoigundua Bwana huyo inafanya kazi. Nitaanza kwa kueleza kidogo maana ya ‘Program Ya Chakula Mwitu’
‘Program Ya Chakula Mwitu’ ni Utaratibu wa namna ya kula chakula cha asili/jadi chenye kiasi kidogo cha carbohydrates (wanga na sukari), kiasi kikubwa cha ptotein na kiasi kikubwa cha mafuta
Ambao lengo lake ni kuchoma mafuta yaliyohifadhiwa ili yabadilishwe kuwa nishati inayoupatia mwili nguvu na kuzuia ongezeko la mafuta huku ukijenga afya bora ya mwili

Program hii sio diet bali ni mtindo wa maisha ‘Life style’ unaolenga kula vyakula rafiki ambavyo vitasaidia ku Program mwili wako usiingie kwenye ‘Insulin Trap’ (mtego wa Insulin) ....
Kwa kuzuia uwepo wa kiasi kikubwa cha glucose na hivyo kuwa na uwezo mkubwa wa kuchoma mafuta.
Program hii inakupatia kitu ambacho unakikosa kwenye kila njia unayoitumia, kitu ambacho kitakusaidia kurejesha shape yako, afya yako, kujiamini na kukusaidia kupungua kiasi chochote unachotaka kupungua
Iwe unataka kupungua kilo 10, 20, 30 na zaidi kwa njia asilia, salama na yenye viwango vya juu vya ubora na kanuni zenye nguvu zilizothibitishwa kuleta matokeo
Sasa tuangalie mambo matano yatakayotokea kwenye mwili wako unapojenga tabia ya kula mlo wenye kiwango kidogo cha carbohydrates na kiwango kikubwa cha protein na mafuta kwa utaratibu unaofaa
Jambo la kwanza ni kwamba utauwezesha mwili wako kuwa na uwezo mkubwa wa kuchoma mafuta yaliyohifadhiwa. Ki vipi?
Unapojenga tabia ya kula mlo wenye kiasi kidogo cha carbohydrates ni wazi kuwa kiasi cha glucose kitakuwa kidogo kuliko mahitaji ya mwili hali ambayo italazimu mwili kutumia yale mafuta yaliyohifadhiwa kama nishati yake.
Jambo hili la mwili kutumia mafuta yaliyohifadhiwa litapelekea mafuta hayo kuendelea kupungua siku hadi siku.
Na unapojenga tabia ya kula mlo wenye kiasi kikubwa cha protini na mafuta ujue kwamba vyakula hivi ili viweze kumeng'enywa ni lazima nguvu kubwa itumike.
Kwa hiyo basi glucose iliyopo haitatosha kwa kazi hii jambo ambalo litalazimu nguvu ya ziada ipatikane kutoka kwenye mafuta yaliyohifadhiwa. Kwa hiyo utakuta mafuta yanatumika na kupungua siku hadi siku.
Na Jambo la pili ni kuwa kupitia program hii unakuwa na uwezo wa kudhibiti hamu na tamaa ya kula vyakula vyenye kiasi kikubwa cha carbohydrates (wanga na sukari)
Hii ni kwa sababu vyakula vyenye kiasi kikubwa cha Protin na mafuta ni vyakula ambavyo vinameng’enywa taratibu. Kwa hiyo ule muda ambao chakula kinameng’enywa huwezi kujisikia njaa badala yake unajisikia kushiba
Hali hii inakusaidia kuepuka kujaribiwa kula vyakula vya carbohydrates kila baada ya muda mfupi. Hapo unakuwa umeepuka kuzalisha kiasi kikubwa cha glucose
Si hivyo tu bali pia ule muda mrefu unaokuwa unajisikia kushiba mwili wako unajipatia nguvu ya kuendelea na kazi zake kupitia mafuta yaliyohifadhiwa. Hivyo mafuta yanaendelea kupungua siku hadi siku
Na jambo la tatu ni kwamba Program hii inakusaidia kujenga misuli yako ya mwili. Misuli ya mwili inajengwa aidha kwa kufanya mazoezi au kula vyakula vyenye kiasi kikubwa cha protini.
Kwa hiyo kupitia Program hii utaweza kujenga misuli zaidi kwa kula vyakula vyenye kiasi kikubwa cha protini. Na endapo utafanya mazoezi pia basi utajenga misuli kupitia lishe na mazoezi
Wakati misuli inajengwa nguvu nyingi inatumika na nguvu hiyo itatoka kwenye mafuta yaliyohifadhiwa. Kwa hiyo kila misuli inapojengwa mafuta yaliyohifadhiwa yanatumika kuupatia mwili nguvu.
Ni kwa namna hii yanapungua siku hadi siku hadi kitambi na manyamazembe kupotea
Si hivyo tu bali pia unapojenga misuli unasababisha nyama za mwili kukaza vizuri na hivyo kuwa na mwili imara wenye nguvu na nyama zilizokaza.
Na jambo la nne, ambalo ni muhimu sana ni kuweka sawa homoni zote mwilini. Ili homoni zikae sawa unahitaji kula vyakula vya asili vyenye protini, mafuta, nyuzilishe, madini na vitamin.
Vyakula hivi ni vyakula vyenye sifa ya kiwango kidogo cha carbohydrates (mboga, matunda, protini na mafuta yenye ubora) kwa kufanya hivi unakuwa umetatua tatizo la kukosekana kwa usawa wa homoni
Na jambo la tano ni kuwa kupitia Program Ya Chakula Cha Mwitu’ Unajenga afya ya mwili na ngozi kwa ujumla nikimaanisha kwamba kila kiungo kinakuwa na uwezo wa kufanya kazi yake vizuri
kama vile ini kutoa sumu mwilini, figo kutoa maji taka maji, mishipa ya fahamu na ubongo kuweka sawa mifumo ya taarifa na kuboresha afya ya ngozi.
Jambo hili linawezekana kwa sababu Utaratibu wa Program ya Chakula Mwitu unajumuisha mlo kamili wenye virutubisho vyote vinavyohitajika mwilini na kuepuka kadiri iwezekanavyo vyakula vyenye kemikali
Hivyo basi kama ungependa kuanza majaribio (ku- beep) ili kuona kitu gani kitatokea, hizi hapa dondoo 8 kuhusu 'Program Ya Chakula Mwitu'.
i) 80% ya mafuta mwilini inaondolewa kupitia Lishe na sio mazoezi magumu.
Watu wengi wanatumia masaa mengi kwenye ‘treadmill’ au gym wakijaribu kupungua. Lakini Wataalam makini wa Lishe, wanariadha na body builders wanajua ‘six-pack’ inatengenezwa jikoni.
Mazoezi ya kawaida ni mazuri ili kujenga afya kwa ujumla. Lakini kama lengo lako ni kupunguza mafuta mwilini kwa kiasi kikubwa, utapata matokeo zaidi kwa kula chakula sahihi tu.
ii) Unaweza kula vyakula unavyovipenda kama vile steki ya nyama, bacon, siagi, mayai, jibini, cream ya maziwa, chocolate na bado ukaondoa mafuta yaliyolundikana mwilini
Kwa hiyo kama uliacha vyakula hivyo kwa sababu ya kukwepa kunenepa na kulinda afya yako Sasa utakuwa na wakati mzuri wa kula na kufurahia chakula chako kupitia Program Ya Chakula Cha Mwitu.
Usiogope kula chakula chenye mafuta mengi na chenye kiwango kikubwa cha protini, cha msingi ni kuchagua mafuta yenye ubora.
iii) Kipaumbele chako kiwe kwenye ubora wa chakula na sio wingi wa chakula.
Kwa kula kiasi kidogo tu cha vyakula asilia (ambavyo havikupitia michakato ya kiwandani) vinavyotokana na mimea na Wanyama na vyenye kiasi kikubwa cha virutubisho vinavyohitajika mwilini. Mwili wako utachoma mafuta yaliyohifadhiwa
iv) Acha kula chakula taka/ chakula mfu.
Hiki ni chakula kisicho na manufaa ya kiafya mwilini. Kwa lugha rahisi ni kile chakula kisicho na virutubisho kama vile vyakula vya kufungashwa vilivyochakatwa na kuongezwa vitu bandia kama vile ladha, rangi na kemikali za kuhifadhia.
v) Hutakiwi kushinda na njaa au kuhesabu calories ili kupunguza uzito
Sahani yenye mlo wa wa chakula asilia kama vile mboga za majani, matunda, nazi na nyama kidogo ina mchanganyiko wa protein, nyuzilishe,mafuta yenye ubora. Mwili wako unahitaji kuridhika na kudhibiti tamaa ya kula kila mara. Ukitaka kuzima njaa, kula chakula asilia.
vi) Usikilize mwili wako na kula chakula wakati una njaa.
Kwenye Program ya Chakula Cha Mwitu, unakula pale unaPojisikia njaa tu, na kama hujisikii njaa mfano, asubuhi, unaweza kuruka mlo huo au kula kiasi kidogo tu
Hii ni kwa sababu unapojisikia njaa, si lazima kuwa mwili wako unahitaji kula, bali unahitaji virutubisho, Unapoulisha chakula kisicho na virutubisho, mwili wako na akili yako kamwe havitatosheka.
Suluhisho ni kula chakula halisia, fresh na kilichokamili chenye kiwango kikubwa cha virutubisho ili kuridhisha njaa yako.
vii) Furahia mlo wako na wenzako kwenye sherehe mbalimbali
Hatuko kwa ajili ya kujiumiza kwa kukaa na njaa au kuhesabu kipimo/ Calories. Tumeumbwa kula na kufurahia kuishi pasipo kunenepa. Kiuhalisia hivi ndivyo imekuwa ikifanyika kwa vizazi na vizazi kabla ya kuanza kufuata ushauri usio sahihi.
Hivyo unapokula nje ya nyumbani, fanya kuwa ni tukio maalum, tumia muda wako na kufurahia mkusanyiko uliopo.
Agiza vyakula mbalimbali kwa staili ya familia kwa kila mmoja kujaribu na kushiriki, hii inasaidia kujisikia kushiba kuliko kula chakula kimoja peke yako
viii) Jiandae na dharura kwa kubeba ‘snack’
Beba mlo mdogo unapotoka kwenda sehemu ili endapo utapata dharura itakayokunyima muda wa kuandaa chakula chako sahihi, utumie akiba yako.
Unaweza kubeba nuts kama korosho, karanga, apple, tango, karoti ,peasi na dark choklate, badala ya kula vyakula vya mitaani,visivyo na sifa kwa afya.
Kwa dondoo hizo chache, utakuwa umeanza kupata picha ya matokeo utakayoyapata kwa kuendelea kujifunza huku akili yako ikiwa tayari kufanikisha lengo lako.
Tazama, "Kujipenda na kujitunza ni zawadi unayoweza kujipatia mwenyewe kila siku. Kila mtu anastahili muda wa kujitunza na kuimarisha afya yake, bila kujali ratiba ngumu au changamoto za maisha.
Huduma yangu ni sehemu ya safari yako ya kujitunza—ninazingatia mbinu za asili ambazo sio tu zinaboresha mwonekano wako wa nje, bali pia zinakufanya uhisi vizuri kwa ndani. Hii siyo kuhusu mazoezi magumu
Bali ni kuhusu kuwa na amani na mwili wako kwa njia salama na ya kudumu."
Hivyo nimeamua kukuandalia darasa jipya kwa lugha ya kishwahili ambapo utajifunza hatua kwa hatua namna ambavyo mtu yeyote mwenye uzito mkubwa, kitambi na manyamazembe anaweza akatumia ‘Program Ya Chakula Mwitu’
Na kuanza kuona mabadiliko ndani ya siku 7 na kuendelea kufurahia mabadiliko ya kushangaza wiki hadi wiki.
Darasa hili nimelipatia jina la …..
Furahia Chakula Mwitu

Darasa Hili Ni Taarifa Mpya, Fursa Ya Kipekee Tofauti Na Madarasa Mengine Ambayo Ushawahi Kujiunga Au Kuyasikia!
Hii ni kutoka na sababu zifuatazo:
Utaratibu wa mafunzo umeandaliwa kwa namna ya kipekee kwa ajili ya kukusaidia kupata kile ambacho unatamani kukipata wakati wote. Hivyo basi Mafunzo yamebuniwa ili......
Kuendana na ratiba yako ngumu ambapo unaweza kujifunza hata ukiwa na ratiba yenye shughuli nyingi kwa kutenga muda kidogo kuendana na ratiba zako za siku na unaweza kutumia Mbinu unazojifunza ukiwa popote na wakati wowote.
Huku ukiwa katika mazingira ya usiri na yanayokuunga mkono na kukutia moyo ili kuhakikisha unapata motisha ya kuendelea kupitia hatua ndogo ndogo ambazo zitaleta mabadiliko makubwa."Hakuna anayehukumiwa au kudharauliwa;
Kwani faragha na usaidizi wa binafsi ni mambo yanayozingatiwa ili usijisikie aibu na uwe huru kufanya mabadiliko ya taratibu na yanayoendana na maisha yako ya kila siku kwani hulazimiki kubadilisha kila kitu mara moja na kujihisi kama unajinyima
Pia mahitaji yako binafsi yakizingatiwa kuendana na mwili wako na hali yako ya kiafya na haihitaji mazoezi magumu au mabadiliko yasiyo salama
Ambapo utapatiwa Mwongozo wa hatua kwa hatua, A- Z ili kuhakikisha unaona mabadilikiko kila wakati kupitia mbinu zinazokufaa na zinazoweza kutekelezeka kwa urahisi,
Hivyo hutakuwa na hofu ya kutofanikiwa kwa kujua kwamba unatekeleza mbinu ambazo ni salama na za asili zilizothibitishwa kuwa na ufanisi si tu kupungua uzito, bali pia kuboresha afya na ustawi wa mwili kwa ujumla.
Na hapo bado sijamaliza kuongelea kila kitu utakachofaidika nacho kwenye darasa hili.
Lakini ngoja nikuelezee mambo machache tu kwenye mengi utakayojifunza kwenye darasa hili kwani darasa langu linatoa suluhisho la kweli la kudumu lililothibitishwa hivyo kuepuka matumizi ya njia zisizo na ufanisi. Utajifunza:
Jinsi Ya Kujiandaa Kisaikolojia ili upate matokeo makubwa, mazuri na ya kufurahisha
Jinsi ya kutumia Mbinu asilia 4 zitakazokusaidia kuyeyusha kitambi na manyamazembe kirahisi kama vile kuyeyusha mafuta ya siagi kwenye kikaango cha moto bila ya mazoezi magumu
Jinsi ya kutumia kanuni 12 za kisayansi ku-Program mwili wako uwe kama mashine inayochoma mafuta muda wote ili kurejesha shape yako ya awali ndani ya muda mfupi kadiri iwezekanavyo
Jinsi ya kuhakikisha kiwango chako cha glucose kinakuwa sawa mwilini wakati wote
Jinsi ya kufanikisha Program Ya Chakula Mwitu’ kwa viwango vya juu sana ili kuzuia usikwame kwa namna yoyote
Jinsi ya kutumia Mbinu 5 za kudhibiti kirahisi kiu ya kula vyakula vyenye kiwango kikubwa cha carbohydrates (vilivyoongezwa sukari na wanga) endapo kiu yako iko juu sana ili kuepuka kutumia nguvu kubwa kudhibiti kiu hiyo
Na zaidi ya yote nitakugeuza kuwa mtaalam wa lishe bora kwa afya ya mwili ili uweze kuwa na mwonekano wa kuvutia na hivyo kujipenda mwenyewe, kujiamini, kuvaa mavazi ya aina yoyote uyapendayo
Huku ukidumisha mahusiano kwenye ndoa yako na kufanya shughuli zako kwa wepesi na urahisi ili kuyafurahia maisha yako yaliyobaki.
Hayo ni baadhi ya mambo machache tu ambayo utajifunza kutoka kwenye darasa hili.
Kiufupi darasa hili ni Daraja la kukuvusha kutoka kwenye mahangaiko na mateso ya muda mrefu ya kukosa njia salama na ya uhakika ya kupungua uzito, kitambi na manyamazembe
Na kukupeleka kwenye ulimwengu mpya wa afya njema, mwili imara wenye nguvu na kuvutia bila ya Maradhi sugu, kitambi na manyamazembe ndani ya muda mchache kadiri iwezekanavyo (mwezi 1 hadi miezi 3 kulingana na ukubwa wa changamoto) huku ukizuia changamoto hizo kujirudia tena kwa maisha yako yote yaliyobakia.
Darasa hili lipo katika mfumo wa Audio (Za kiswahili) na picha ambapo nakuelekeza hatua kwa hatua ukiwa unasikiliza mwenyewe na kuona jinsi ya kutekeleza maelekezo kupitia simu yako (smart phone) au kompyuta
Kwa nini nimefanya darasa liwe katika mfumo wa Audio na picha? Kwasababu Audio na picha ndio njia pekee rahisi ya kumfundisha mtu akiwa anaona na kusikia anachotakiwa kufanya tofauti na kusoma kitabu
Katika Darasa hili ninakupatia mwongozo kwamba hapa unafanya hivi na hapa inakuwa hivi. Kwahiyo kwa kufanya hivyo itakuwa rahisi sana kwako kufanya utekelezaji wa haraka wa kile utakachojifunza na kufanya upate matokeo ya haraka.
Kwa kusaidia mwili wako kuwa na kiwango kizuri cha glucose kwenye damu kisicho na madhara ya kukusababishia uzito mkubwa, kitambi na manyama zembe na uepuke kuingia kwenye mtego wa Insulin
Wanafunzi wangu wengi wa umri tofauti, changamoto tofauti na kutoka maisha mbalimbali wameona mabadiliko makubwa ndani ya wiki chache za kwanza za programu, si kupungua tu uzito bali afya zao kubadilika pia.
Kuamini ninachokisema hawa hapa ni baadhi ya wahanga ambao hawakuamini kama Kupitia Njia asilia tu wangeweza kupungua
Ngusekela Daniel: Mbeya
Asante sana madam, nilikuwa na kilo 170 utashangaa sana, sasa nina 132 ,nimeshaondoa 28 na bado nasonga mbele. Hata pete ya arusi ilikuwa imebana mpaka ikabidi nikakate kwa sonara. Sasa hivi inazunguka kwenye kidole. Uwii, sijiamini kabisa kuwa ni mimi. Thanx teacher, bravo.
Winnie Alpha: Da es Salaam
Yaani madam ubarikiwe sana maana sina neno zuri zaidi, nikijiona najipenda mwenyewe tamaa yangu ya kuvaa suruali na kuchomekea imetimia maana sijawahi kuvaa kwa vile ilikua haikai ,tumbo kama lote. Sina neno zuri zaidi ya asantee umebadilisha maisha yangu kabisa
Valerian mushi: Kilimanjaro
Nimepona miguu, uchovu umeisha kabisa, ninakuwa na hamu na baba watoto wangu
Tumbo limepunga sanaaa, Nimetimiza lengo langu nilikua na kilo 83 sasa hivi nina 62 . Nina furaha sana. Picha ya kabla naogopa kutuma tumbo lilikuwa kubwa mno
Asha Mwinjuma: Tanga
Eti jamani naulizwa sasa hivi unapakaa nini? nawajibu napakaa chakula cha mwitu.
Nafurahi nimeweza kujizuia kula ovyo ovyo, nimejua kupangilia milo ya siku nzima, nguo nilizozikatia tamaa sasa ninazivaa, kutoka kilo 123 sasa nina 102 ndani ya miezi 2 bado nasonga mbele hadi nifikishe kilo 75
Sarah Dumbe: Dar es salaam
Baada ya siku 13 nina matokeo yafuatayo; hamu ya kula vyakula vingi sana imepotea, vinywaji kama soda ndio kabisaa sina hamu navyo, napata usingizi mzuri, nilianza na kilo90 sasa nina 84 , kuna magauni 3 yamenipwaya . mwalimu kazi iendelee
Wellu kiyula: Dodom
Ninakula kama binti wa mfalme cha kushangaza baada ya siku 12 nimepungua kilo 6 kutoka 90 hadi 84, Uwiiii, siamini macho yangu yani nimesota na dawa za gharama kubwa mno lakini hapa nakula vizuri na bado nimepungua ndani ya muda mfupi hivi. Mungu akulinde teacher Rehema na akupe haja ya moyo wako.
Denice Mboya: Morogoro
Nimerudisha tabasamu langu, sichokichoki ovyo, mwili umekuwa mwepesi ,nimepungua kilo 8 ndani ya wiki 4. Nyama za kwenye mbavu kwishne, nilikuwa na matairi balaa.brazzier zimepwaya. Hakika nimepata ushindi kwa kile nilichokuwa nimekusudia.
Joyce John: Lindi
Hakuna kama wewe, uuuuwi! Nishajaribu sana walimu na products za gharama kubwa mtandaoni ilishindikana. Matokeo ni makubwa sasa ninachomekea sasa, napitapita mitaani kama panya ili kila mtu anione. Upewe maua yako mwalimu
Winna Freddy: Mwanza
Kupitia program hii nimeweza kupunguza kilo 23, nimekuwa miss kwelikweli. Nguo nilizokuwa navaa miaka kumi iliyopita ndio sasa zinanitosha vizuri. Kwa miaka kadhaa nilikuwa nahangaika kupungua angalau kilo 2 tu na ikashindikana, kwa program hii kupungua kilo 23 ni muujiza. Juzi nilienda arusini nikiwa na furaha kwa kuwa nilijiona nimependeza hadi kila mtu ananiuliza kulikoni?
Joyce Kiluwa: Manyara
Mwili wangu umekuwa mwepesi, maradhi ya mgongo, kiuno, kichwa, miguu yameisha, nilikuwa nahema sana nikipanda ngazi sasa hivi nipo fresh, napanda bila kushika popote, nilikuwa siwezi kuinama kudeki lakini wiki nzima dada wa kazi kaondoka mimi sasa hivi ndio msichana.kasura sasa, ngozi lainii na yenye mvuto kama kachanga. Nimepungua hadi wenzangu wananitamani. Napiga kazi vibaya mno hadi Mr. anashangaa.
Sarah John: Dar es salaam
Nilikuwa na waalimu zaidi ya kumi nikawaacha, maana sikufanikiwa kupungua. Hapa nimepungua kilo 20, tumsikilize mwalimu Rehema na tuache mazoea ya tulikotoka
Amina Ally: Zanzibar
Asante sana mwalimu kutoka 110 hadi 82 haikuwa rahisi, kwa msaada wa Mungu nimeweza , nipe mwezi 1 niondoe kilo 4 . nimeishi na uzito kwa miaka 11 lakini nilipoamua kutoka moyoni nimeweza. Nashukuru mwalimu.Ninaweza kujiona kiuno changu kilivyokatika sasa na mapaja yalivyopungua.
Ummy Salimu: Zanzibar
Program yako ni rahisi kufuata kuliko kitu chochote kile, yani ninashiba huku napungua vizuri. Japo nilijifungua kwa operation lakini nimepungua vizuri na nyama za tumbo zimekaza kabisa.
Darasa Hili Linagharimu kiasi Gani?
Kabla sijakuambia bei ya kujiunga na darasa hili ningependa wewe mwenyewe ujipangie bei
Unajipangia bei kwa darasa ambalo ni Daraja la kukuvusha kutoka kwenye mahangaiko na mateso ya kukosa njia salama na ya uhakika ya kupungua uzito, kitambi na manyamazembe…
Na kukupeleka kwenye Neema ya suluhisho la uhakika, salama na la kudumu kwa kukuhakikishia afya njema, mwili imara wenye nguvu na kuvutia bila ya Maradhi sugu, kitambi na manyamazembe
Unajipangia bei kwa darasa ambalo Mafunzo na mbinu utakazojifunza zitaanza kukupatia mabadiliko ndani ya siku 7 na utaendelea kutumia mafunzo na mbinu hizo kwa maisha yako yote yaliyosalia
Unajipangia bei kwa darasa ambalo mbinu nitakazozifundisha nimeweza kuzipata kwa gharama isiyopungua milioni 2 (2,000,000/=)
Unajipangia bei kwa darasa ambalo mbinu nitakazokufundisha huwezi ukazipata sehemu yoyote ile kwa hapa Tanzania tofauti na kwangu
Ukijipangia 800,000/= utakuwa upo sahihi japo mimi aliyenifundisha mbinu hizi akisikia nakuuzia kwa hiyo bei ataumia sana na huenda ataniona mimi nimechanganyikiwa maana 800,000/= ni ndogo sana ukilinganisha na faida unazozipata kupitia mbinu nitakazokufundisha
Lakini unajua cha kushangaza ni nini? hutalipia hiyo 800,000/=
Pesa utakayolipia hata nusu ya hiyo 800,000/= haifiki.
Nina mpango wa kuuza darasa hili kwa 350,000/=
Lakini kama utalipia leo hii au kama utakuwa miongoni mwa watu 200 wa kwanza kujiunga kwenye darasa nitakupunguzia bei kwa 57%
Kwa hiyo badala ya 350,000/ = utajiunga na darasa hili kwa
200,000/= TU
Kuna sababu 3 kwa nini natoa punguzo la bei.
Na kabla sijakwambia sababu hizo nikukumbushe kwamba watu 200 wakishajiunga kwenye darasa hili OFA hii ya punguzo la bei haitakuwepo tena.
Watu 200 wanaonekana wengi sana lakini kumbuka sasa hivi ukurasa huu unasomwa na watu zaidi ya 7000 wenye matamanio ya kupungua uzito na kuondoa kitambi na manyamazembe kwa njia ya uhakika na salama
Sijui ni kwa muda gani watu 200 watakuwa wamejiunga kwenye darasa. Pengine huenda baada ya siku 5 au chini ya hapo watu hao 200 watakuwa tayari wameshajiunga kwenye darasa kulingana na kiu yao ya kumaliza changamoto hiyo
Kwahiyo epuka kujutia baadae utakapokuta bei imepanda. Ni vyema ukajiunga kwenye darasa sasa hivi ili uwe miongoni mwa watu wa kwanza ambao wataanza kupata matokeo
Sababu Za Mimi Kutoa Punguzo La Bei Kubwa Namna Hiyo
Kuna sababu 3 na ni rahisi kuzielewa
i) Lengo langu ni kuhakikisha kwamba wanawake wengi zaidi wanapata fursa ya kujiunga na darasa langu na kubadilisha maisha yao. Nataka kila mwanamke ajisikie kuwa na uwezo wa kuchukua hatua katika safari yake ya afya bila kikwazo cha kifedha.
ii) Nataka kujenga jamii ya wanawake wanaoungana na kusaidiana katika safari hii. Punguzo la bei linaweza kuwavutia wanawake wengi zaidi, na hivyo kuunda mazingira ya ushirikiano na motisha.
iii) Ninajua kwamba huduma zangu zina ufanisi. Kwa punguzo hili, ninaamini kuwa wengi watapata matokeo chanya na kutangaza huduma yangu kwa wengine, hivyo kusaidia kueneza taarifa kuhusu mbinu zangu za asili na salama.
Kwa maelezo rahisi ni kwamba punguzo hili lina faida pande zote 2. Kwako na kwangu
Kwa hivyo, usikose fursa hii! Jiunge na darasa langu kwa bei hii nafuu na anza safari yako ya kubadilisha maisha.
Punguzo hili ni la muda mfupi, hivyo chukua hatua sasa ili usikose fursa hii ya kipekee!
Punguzo hilo la bei mpaka 200,000/=
Ni punguzo kwa watu 200 wa kwanza ambao watajiunga kwenye darasa [kwa hiyo wakifika watu 200 hutoweza kupata punguzo hili la bei kwa hiyo ni vema uwahi]
Kumbuka, kila siku ni fursa mpya ya kubadilisha maisha yako, lakini pia ni siku unayoweza kupoteza. Ili usijute baadaye Jiunge na darasa langu sasa hivi
Kwa kuwa Ninataka uwe na uhakika wa 100% unapochukua hatua ya kujifunza kwenye darasa langu, ninatoa dhamana (guarantee) ya siku 30 na hii ni kwa sababu nina uhakika wa mbinu zangu katika kuleta matokeo.

Guarantee hii ipo hivi...
Lipia darasa hili sasa hivi, fanyia kazi siku 30 mfululizo ambao ni muda wa kutosha wa kufanyia kazi nitakachokufundisha na kuona mabadiliko.
Iwapo kwa sababu yoyote ile ndani ya siku 30 utakuwa hukuridhishwa niambie kupitia namba ya simu ambayo itakuwepo kwenye receipt ya malipo utakayokuwa umefanya nami nitakurudishia hela zako zote 100% bila kinyongo chochote. Hivyo huna cha kupoteza
Kwanini natoa guarantee hii ya kukurudishia 100% ya hela zako zote?
Ni kwa sababu
Hii ndiyo sababu ninatoa dhamana hii – kwa sababu ninajua matokeo yako yanaweza kubadilisha maisha yako.
Hivyo Fanya Uamuzi Leo! Jiunge na darasa langu kwa uhakika wa dhamana hii. Usikose nafasi hii ya kuondoa kitambi na uzito kwa njia salama, huku ukiwa na amani ya akili.
Nina uhakika 100% utakavyojionea mwenyewe kwenye darasa hili namna ya kutumia ‘Program Ya Chakula Cha Mwitu’ kugundua mbinu ambazo huwezi kuzipata sehemu yoyote kwa hapa Tanzania za kukufanya upate matokeo ya ndoto zako.
Na utakavyojifunza kuepuka Makosa ambayo ndio chanzo cha wote wanaopunguza uzito, kitambi na manyamazembe kupoteza muda na fedha kwa njia zisizo na uhakika
Wewe mwenyewe utakuwa unasema kimya kimya moyoni inabidi niongeze bei ya darasa hili hata mara kumi zaidi maana mbinu ulizojifunza kutoka kwenye darasa hili zitakufanya uwe mrembo na mvuto wa kipekee
Huamini kama inawezekana? Nijaribu.
Ninakuongezea pia na bonus hizi (BURE KABISA)
Hivi ni vitabu (soft copies au PDF)
1. Milo yenye nguvu ya kuchoma mafuta
2. Chati ya utaratibu wa kila siku ili kurahisisha ratiba yako ya siku
Utaungwa kwenye darasa la usaidizi ‘Badili Mwili Wako Kwa Chakula Mwitu’
Ili kupatiwa usaidizi zaidi kwa kujibiwa maswali yako yote
Je, una swali? Huenda likawa limejibiwa hapa?
Vipi kama Program haitafanya kazi kwangu?
Ninajua utaratibu huu unafanya kazi kama ambavyo umefanya kwa wengi walioutumia na kupata matokeo ndani ya muda mchache. Hata hivyo ninaelewa bado unaweza kuwa na mashaka na kutokana na hilo ninataka kufanya kila niwezalo ili uwe huru kufanya maamuzi kwa sababu ninaweza kuleta mabadiliko kwenye maisha yako na nina amini itakuwa hivyo. Na kutokana na hilo ndio sababu natoa guarantee ya siku 30 za kurudishiwa pesa yako yote., kwa sababu yoyote ile endapo utatekeleza maelekezo yangu halafu usiridhike , tafadhali wasiliana nami nikurudishie pesa yako yote . ni rahisi hivyo.
Je, nitahitaji kujinyima kula kupitia Program hii?
Hapana hutahitaji hata kidogo, si kwamba tu program yangu inaruhusu kula vyakula vingi vyenye carbohydrates bora, mafuta na protein mara nyingi zaidi bali pia kuna utaratibu wa siku ambazo unaweza kula chochote unachotaka kula na ukaendelea kupata matokeo mazuri
Je, program hii imeandaliwa kwa ajili ya wanawake na wanaume?
Njia za Program Ya Chakula Cha Mwitu inafanya kazi kwa jinsia zote 2, hata hivyo ziko tofauti kidogo tu kwenye baadhi ya mbinu. Mimi kufundisha wanawake tu haimaanishi kuwa inafanya kazi kwa wanawake tu.
Je, Program hii imeandaliwa kwa namna ya kupunguza mafuta au kujenga misuli?
Mbinu zinazotumika kwenye Program ya Chakula Cha Mwitu zinafanya kazi kote kote, kupunguza mafuta kujenga na kuimarisha misuli. Ukweli ni kwamba unapojenga misuli matokeo ni kupunguza mafuta. Mfano ukitaka kujenga shape nzuri au six pack abs, mazoezi hayatakuwa na faida isipokuwa tu kama utachoma mafuta yanayofunika misuli tumboni. Utajifunza ina maanisha nini tukizungumzia Lishe na nguvu ya chakula katika mabadiliko
Umri wangu hauko kwenye miaka ya 20 wala 30, je, Program hii bado itafanya kazi?
Ndiyo! Watu wengi katika umri wa miaka 50 na 60 wameshuhudia mabadiliko makubwa kwa kutumia program hii. Program imeandaliwa ku rekebisha kasi ya metaboliki bila kujali umri.
Ninataka kuanza kufanyia kazi program sasa hivi; Je, nitatakiwa kusubiri hadi utume taarifa zote hizi kabla sijaanza?
Hapana. Program yote itakufikia mara moja kupitia mtandaoni ndani ya saa 24 mara tu baada ya kulipia, hakuna gharama za kutuma, hakuna kusubiri kwa ajili ya kuanza program
Mimi ni mzee/ Nina uzito mkubwa/ shape (umbo) limeharibika. Je, Program hii itakuwa ngumu sana kwangu kutekeleza?
Hapana kabisa – Ni rahisi mno. Utaratibu wa Lishe unafanya kazi kwa kila mmoja. Mafunzo na mbinu zote za lishe zinaweza kutumiwa na kila mtu kuanzia vijana wanaotaka kuwa na miili yenye nguvu na imara hadi wazee (bibi na babu) ambao wanapenda kujisikia vizuri kiafya.
Je, ninahitaji kujiunga na gym au ninaweza kufanya mazoezi nyumbani?
Ni uamuzi wako. Mimi siendi gym na hata wanafunzi wangu wengi hawaendi gym, wanafanya shughuli au mazoezi ya kujichangamsha nyumbani.
Kiuhalisia unaweza kupata matokeo mazuri kwa kufanya mazoezi yaliyo mengi kwa kutumia mwili wako tu bila kifaa chochote. Na kama una hali isiyohitaji mazoezi, unapungua bila mazoezi yoyote.
Je, Program hii inahusisha mbinu za Lishe na utaratibu wa kula ili kuondoa mafuta au ni kuhusu mazoezi tu?
Utaratibu wa Lishe ndio hasa kilicho muhimu kwenye Program hii. Kuwa na uelewa mzuri kuhusu Lishe ni muhimu sana kama unataka kupungua uzito na kuwa na tumbo bapa.
Je, program hii itahitaji ninunue virutubisho lishe vya gharama au vidonge vya kupunguza uzito?
Hapana , hata kidogo. Mimi ninachukulia kama lishe za ziada (supplements ) nyingi na vidonge (diet pills) kama kupoteza pesa tu. Vinaweza kukusaidia lakini ni kwa muda mfupi tu. Ukweli ni kwamba huhitaji supplements ili kuwa na mwili uupendao. Unachohitaji ni Mchanganyiko wa vyakula vyenye virutubisho munimu kwa afya ya mwili.
Je, kama mimi sili nyama (vegetarian) bado ninaweza kutumia Program hii?
Ndiyo, bado unaweza kutumia kanuni za kuondoa mafuta yaliyozidi mwilini na ukapata matokeo makubwa. Utahitaji tu kufanyia mabadiliko baadhi ya mifano. Hata hivyo maadam umechagua kuondoa vyakula vinavyotokana na wanyama, utahitaji kuwa makini zaidi kupata vyakula vinavyotokana na mimea vyenye kiwango kikubwa cha protein.
Siwezi kula ngano au chochote chenye gluten. Bado ninaweza kutumia Proram hii?
Ndiyo, tena utakuwa hatua moja mbele zaidi
Mazoezi yanachukua muda gani kwenye Program yako na ni mara ngapi kwa wiki nitayotakiwa kufanya?
Utaratibu Wa Program Ya Chakula Cha Mwitu kiuhalisia unalenga zaidi kula kwani 80% ya matokeo utakayoyapata yatatokana na kile unachokiingiza mwilini na sio unachokifanya. Japo mazoezi yaliyopo yatakusaidia kuongeza kasi ya kupara matokeo kwa haraka zaidi.
Mazoezi ya kawaida yanaweza kuchukua kati ya dakika 15 hadi 45. mara tatu au zaidi kwa wiki kutegemeana na aina ya zoezi
Je, kama mimi nimejifungua kwa operation bado naweza kutumia Program hii?
Ndiyo. Program hii ni salama kwa afya yako kwani haikulazimu kufanya mazoezi magumu. Sehemu kubwa ni Lishe ambayo itakusaidia pia kupona haraka.
Je, naweza kutumia Program hii nikiwa bado nanyonyesha?
Ndiyo. Unachohitaji ni mlo kamili wenye virutubishoo kwa wingi ambavyo utavipata kupitia Program hii
ILI KUJIUNGA NA DARASA HILI FANYA HIVI SASA :
Kabla nafasi 200 hazijajaa na kusababisha ukose punguzo la bei hakuna wakati mwingine tofauti na sasa hivi wa kujiunga kwenye darasa hili.
Tazama, kama mama wa familia unategemewa kwa mambo mengi ya kuendeleza familia yako. Kila mmoja anatamani kukuona ukiwa mama mchangamfu, anayejituma na kulea familia yake muda wote.
Au uko tayari kuendelea kupoteza kujiamini na kupoteza mvuto, kulala kitandani kwa maradhi, kunung’unika muda wote kwa uchovu, kuhudumiwa kama mtoto na hata kutumia sehemu kubwa ya bajeti ya famili yako kwa kujitibu?
Wewe ndiye mwenye maamuzi.
Kujiunga kwenye darasa hili ni rahisi sana.
Ili ujiunge kwenye darasa inatakiwa ulipie kwanza halafu ukimaliza kulipia nitumie uthibitisho wa malipo kwenye whatsapp yangu ili uanze mafunzo
Malipo yote yanafanyika kwa njia ya M-pesa au CRDB Bank.
Namba ya M-pesa (Voda) ni 0752267000 jina ni REHEMA RAPHAEL PAUL
Namba ya Account ya CRDB ni 01J2008017800 jina ni REHEMA RAPHAEL PAUL.
Namba ya kutuma uthibitisho wa malipo whatsapp ni 0752267000
Ahsante kwa muda wako.
Ni mimi,
Mwalimu Rehema
P.S: Kama nilivyokwambia punguzo la bei la 200,000/= ni kwa watu 200 tu wa kwanza baada ya hapo bei itabaki ile ile ya 350,000/=
Usiendelee kusubiri kujiunga kwenye mafunzo kwa sababu bei itapanda muda wowote.
This site is not a part of the FacebookTM website or FacebookTM Inc. Additinally, this site is Not endosed by FacebookTM in any way. FACEBOOKTM is a trademark of FACEBOOKTM.inc